HABARI, BIASHARA, MUSIC, SIASA, MICHEZO,

Tuesday, 18 October 2016

Hali ya Siasa ARUSHA Yawa sinema kwa                       Wananchi wa Jiji Hili


*MKUU WA MKOA WA ARUSHA  AMBAYE NI MTEULE WA RAISI AZUIA MBUNGE LEMA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA ENEO LA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA WATOTO JIJINI ARUSHA*
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mkuu huyo azuia Mbunge Godbless Lema kuweka jiwe lamsingi katika eneo litakalojengwa hospitali ya kisasa ya Mama na watoto chini ya msaada wa shirika lisilo la kiserikali la Maternity Africa muda huu.. Zoezi hilo limesimama baada ya Mkuu kuwaambia wafadhili hao kuwa eneo hili halikutolewa na Mawalla bali nila mke wa Mbunge na hivyo kupelekea wafadhili hao kubaki na butwa na kutokujua la kufanya.
Katika hali nyingine Mkuu ametoa masharti kwashirika hilo kuwa wakitaka kusimika jiwe la msingi nilazima wahakikishe mbunge Lema hazungumzi wala mkurugenzi wa ARDF ambaye anasimama kukabidhi eneo hili.
Mpaka sasa tuko eneo la tukio pasipo muafaka maalum.
Huu ni muendelezo ya vita ya kisiasa ya jijini Arusha ambayo inazuia shughuli za kimaendeleo ambazo nifaida za wananchi na sio wanasiasa.


No comments:

Post a Comment