YANGA BANA! HEBU ISOME HII HABARI YA CEO MPYA WA CLAB HIO
WAKATI mashabiki na wanachama kadhaa wa Yanga wakilalama kuondokewa
na kocha wao kipenzi, Hans van Pluijm, uongozi wa klabu hiyo
unakamilisha taratibu za kuingia mkataba na Mtendaji Mkuu mpya wa klabu
hiyo Mfaransa, Jerome Dufourg, ambaye rekodi yake inatisha.
Mtendaji huyo mpya pindi atakapoajiriwa atakuwa na mamlaka ya juu
kabisa katika mambo yote ya uendeshaji wa klabu, ambapo taarifa za ndani
ambazo DIMBA Jumatano limezipata zinadai kuwa yuko karibu kusaini
mkataba wa miaka mitatu.
Dufourg, raia wa Ufaransa, ni miongoni mwa watu wanaotambulika na
Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) kutokana na kuwa na wasifu (CV) wa
juu katika mambo ya soka.
Mfaransa huyo kijana mwenye umri wa miaka 30, ana shahada ya juu ya
Fifa katika uongozi wa soka kuhusiana na uchumi pamoja na utawala.
Katika nchi za Afrika, amewahi kufanya kazi Shirikisho la Soka nchini
Rwanda (FERWAFA) pamoja na klabu ya FC Talanta ya Ligi Daraja la Pili
nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment