HABARI, BIASHARA, MUSIC, SIASA, MICHEZO,

Thursday, 24 November 2016






Huku maeneo mengi ya dunia yakihangaika na magereza yaliyojaa wafungwa kupita kiasi, Uholanzi ina tatizo tofauti. Uhaba wa wafungwa.
Katika kipindi cha chini ya miaka 19, magereza yamefunga shughuli zake na mengine zaidi yamepangwa kufungwa mwaka ujao. Ni vipi hili liliwezekana - na kwa nini baadhi ya watu wanafikiri ni shida?
Harufu nzuri ya kupendeza ya vitunguu inanukia, kupitia mlilango ya mahabusu na katika jengo zima. Jikoni wafungwa wanaandaa chakula chao cha jioni. Mwanamume mmoja aliyeko upande mmoja wa jiko anakata mboga.
"Nilikuwa na miaka sita ya kujifunza sasa nina uelewa zaidi wa shughuli hii!" alisema.
Ni kazi yenye kelele kwa sababu kisu kimefungwa kwenye nyororo ndefu iliyofungwa juu.
"Hawawezi kuchukua kisu hicho mikononi ," anasema Jan Roelof van der Spoel, naibu gavana wa gereza la Norgerhaven, lenye ulinzi mkali lililoko kaskazini mashariki mwa Uholanzi. "
"Lakini wanaweza kuazima visu vidogo vya jikonikama wakitoa vitambulisho vyao ili tufahamu ni nani ana nini."
Baadhi ya wanaume hao wamefungwa kwa kufanya makosa ya ghasia na wazo kwamba watembee na visu ni suala linalotia shaka. Lakini kujifunza kupika ni moja tu ya njia ambazo gereza husaidia wafungwa kurejea katika maisha ya kawaida mara baada ya kufunguliwa
"Katikka magereza ya Uholanzi tuanaangalia kila mmoja," anasema Van der Spoel.
"Kama mtu fulani ana matatizo ya mihadarati tunatibu hali yake, kama ni wenye hasira tunawapatia ushauri wa kudhibiti hasira zao , kama wana matatizo ya pesa tunawapatia ushauri nasaha. Kwa hiyo tunajaribu kuondoa kile kinachosababisha mtu afanye uhalifu . Mfungwa mwenyewe lazima awe na utashi wa kubadilika lakini njia yetu imewafaa sana. Kwa zaidi ya miaka 10 , kazi yetu imeboreka zaidi na zaidi.''
Wafungwa wanaofuata maelekezo hatimaye hupewa kifungo cha miaka miwili na msururu wa mafunzo katika mpango wa kuwarejesha katika hali ya kawaidi . Chini ya 10% hurejea gerezani baada ya kuachiliwa huru.
Hewa safi ni muhimu kwa hiyo wafungwa huruhusiwa kutembea wakisindikizwa hadi maktaba , kwenye kliniki ama mgahawa na hilo huwasaidia kuendelea na maisha ya kawaida punde wanapomaliza kifungo cha gerezani.
Muongo mmoja uliopita Uholanzi ilikuwa ni mojawapo ya nchi zenye kifungo cha muda mrefu zaidi barani Ulaya, lakini sasa inadai kuwa nchi yenye wafungwa wachache zaidi, yaani wafungwa - kati ya watu 100,000 , ikilinganishwa na wafungwa 148 Uingereza na Wales.
Lakini mpango wa kutoa ushauri nasaha si sababu pekee iliyosababisha kupungua kwa watu katika magereza ya Uholanzi - kutoka wafungwa 14,468 mwaka 2005 hadi wafungwa 8,245 mwaka jana - kiwango hicho kikiwa sawa na asilimia 43.
Kupungua zaidi kwa idadi hiyo mwaka 2005 kulisababishwa kwa sehemu kubwa na kuboreshwa kwa upekuzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amsterdam-Schiphol, ambako kulisababisha kubainika kwa idadi ya wauzaji wa mihadarati kukamatwa wakiwa wamebeba cocaine.
Angeline van Dijk, Mkurugenzi wa huduma za magereza nchini Uholanzi, anasema magereza sasa yanatumiwa kuwahifadhi wale ambao ni hatari sana kuachiliwa, ama wahalifu waliomo hatarini wanaohitaji usaidizi wakiwa ndani ya gereza.
"Wakati mwingine ni vyema kwa watu kukaa katika kazi zao, wakae na familia na kufanya adhabu kwa namna nyingine," anasema kulingana na uzoefu wake wa kazi hiyo.
"Tuna hukumu za muda mfupi za gerezani na kupunguza viwango vya uhalifu hapa Uholanzi, kwa hiyo hili linaacha magereza yetu kuwa matupu ."
Mojawapo ya gereza lililokosa watu liligeuzwa kuwa Hoteli ya kifahari kusini mwa mji wa Amsterdam, ni hoteli ya nne kwa kuwa ghali, ikipewa majina ... The Lawyer, The Judge, The Governor na The Jailer.
Lakini mengine yaligeuzwa kuwa vituo vya kuwapokea wahamiaji, na kutoa ajira kwa baadhi ya walinzi wa zamani wa magereza.
Azma ya kulinda ajira za magereza imetoa suluhu ya kushangaza - kuletwa kwa wafungwa wa kigeni kutoka nchi za Norway na Ubelgiji

No comments:

Post a Comment