Saturday, 26 November 2016
SAMATA USO KWA USO NA POGBA!
KIKOSI cha KRC Genk cha nchini Ubelgiji anachochezea Mtanzania Mbwana Samatta, kimefanikiwa kutinga hatua ya mtoano ya michuano ya Europa League baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rapid Wien.
Bao pekee la Genk lilifungwa na mshambuliaji hatari wa kikosi hicho, Nikolaos Karelis, dakika ya 11 ya kipindi cha kwanza, mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Laminus Arena wa Genk.
Ushindi huo umeifanya Genk kufikisha jumla ya pointi tisa kileleni sawa na Atletic Club ya Hispania iliyopo nafasi ya pili, zikitofautiana wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa kwenye kundi F.
Nayo Rapid Wien inakamata nafasi ya tatu wakati Sassuolo ya Italia ikiburuza mkia.
Katika mchezo huo Samatta aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Karelis na kuonyesha uwezo mkubwa.
Kutinga kwa Genk katika hatua hiyo kuna maana kubwa kwa Mtanzania huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki michuano hiyo mikubwa Ulaya.
Hiyo ni fursa kwa Samatta kuzidi kuonyesha uwezo mkubwa kwani huenda akazivutia timu kubwa barani Ulaya zikamsajili, ikizingatiwa kuwa zipo timu kama Manchester United zinashiriki ligi hiyo.
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment