MABAHARIA WALIO TEKWA SOMALIA 2012 WAACHIWA HURU
Kundi la mabaharia ambao
waliachiliwa huru Jumamosi baada ya kuzuiliwa na maharamia kwa miaka
mitano nchini Somalia walikula hata panya ili waishi, mmoja wao amemwambia Mwandishi wetu, kutoka Ufilipino amesema walikuwa wanapewa
maji kidogo sana na walijihisi kama "wafu waliokuwa wakitembea" kufikia
wakati wa kuachiliwa huru kwao.
Mabaharia hao walitekwa wakiwa
kwenye meli mwaka 2012 kwenye pwani ya Ushelisheli na wakapelekwa
Somalia bara na kuzuiliwa mateka.Waliachiliwa huru Jumamosi. Taarifa zinasema waliokuwa wanawazuilia mateka walilipwa kikombozi.
No comments:
Post a Comment