Prof. Mbarawa atangaza vita na Madereva. Isome habari hii hapa http://salymjuma.blogspot.com
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametoa agizo kwa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kuwabaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wote wa malori ya mchanga na kokoto watakaobainika kutofuata sheria za ubebaji wa bidhaa na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo juzi mkoani Kigoma katika ziara yake ya kukagua Barabara ya Kidahwe-Kasulu yenye urefu wa kilomita 50, ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu ya barabara kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla, hivyo haitamvumilia mtu yeyote atakayebainika kuharibu miundombinu hiyo kwa makusudi.
No comments:
Post a Comment