HABARI, BIASHARA, MUSIC, SIASA, MICHEZO,

Tuesday, 25 October 2016


Ukatili kwa Watoto wazidi kufanyika Arusha

Mkurugenzi wa Shirika la Women in Action for Development (WIA), Elizabeth Mosha.


Jiji la Arusha limeendelea kushuhudia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto unaofanywa na walezi pamoja na wazazi ambapo watoto wawili wa familia tofauti wamethibitika kufanyiwa kitendo cha ubakaji na baba zao.
Imeelezwa kuwa kuendelea kwa vitendo hivyo vya kikatili kunachangiwa na baadhi ya madaktari kutofuata maadili ya kazi zao sambamba na kutochukuliwa hatua za kisheria kwa watuhumiwa wa vitendo hivyo.
Kwa Mujibu wa Bi Maria Thomas, ambaye ni mratibu wa idara ya elimu katika shirika linalo jihusisha na maendeleo ya wanawake na watoto yatima Women in Action for Development (WIA) Anaeleza jinsi walivyogundua kufanyiwa kitendo hicho kwa mtoto Janeth mwenye umri wa miaka 6 wakati akiwa shuleni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Women in Action for Development (WIA), Elizabeth Mosha, amesema kuwa wataendelea kusimamia kesi hiyo mpaka mtuhumiwa atiwe hatiani ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaowafanyia vitendo hivyo watoto.
Mtuhumiwa aliyefanya kitendo hicho cha kikatili anayefahamika kwa jina la Jumanne Saidi mwenye umri wa miaka 59 mkazi wa kwa Morombo Jijini Arusha bado haijajulikana hatma yake huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo
Aidha katika tukio lengine la ukatili wa kijinsia kwa watoto, mtoto mwenye umri wa miaka 7 amefanyiwa kitendo hicho na baba yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Majimoto Huseni mwenye umri wa miaka 38 ambapo inaelezwa kuwa mama mlezi wa mtoto huyo kutokuwa na maelewano na mumewe kwa kipindi kirefu.
Tukio hilo ni la 5 kuripotiwa katika kituo cha Women in Action for Development (WIA).

No comments:

Post a Comment