Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR Mageuzi (2010-2015) na baadaye kuhamia chama cha ACT Wazalendo mwaka 2015 Moses Machali, leo ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)
Katika
taarifa yake aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari, Machali amesema
sababu kubwa ya uamuzi huo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
serikali ya awamu ya tano chini uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli
pamoja na utendaji makini wa Waziri Mkuu wake Mhe. Kasim Majaliwa.
"Mimi Moses Joseph Machali niliyefanya sana siasa za upinzani hapa nchini na niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii; niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ninaamua kujiunga na watu wanaoonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi yetu Tanzania". Amesema
Amesema mambo yote aliyoyapigania, kwa sasa yametekelezwa kwa kiasi kikubwa na haoni sababu za kupingana na yale aliyoyapigania.
"Miradi kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona wapinzani; sasa yanafanyika". Amesema Kuhusu malalamiko ya ugumu wa maisha Machali amesema "Hata kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu na suala la kudhibiti wapiga dili wa fedha na mali za umma bali tukubali kwamba wapiga dili waliozoea kupiga dili na kuziingiza fedha walizopiga katika mzunguko siyo jambo la msingi katika kujenga uchumi imara"
Machali pia ametoa ushauri kwa wafuasi wa vyama vya upinzani kuacha kuamini kuwa mambo yote yanayofanywa na CCM ni mabaya
"Tuachane na siasa nyepesi za kutaka kuona kwamba mazuri ni yale yanayofanywa na wapinzani huku mambo hayohayo yakifanywa na CCM yaonekane hayafai na kutajwa kuwa ni ya hovyo. CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga mkono".
Amehitimisha kwa kusema "Kwaherini upinzani nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo.
Hii si mara ya kwanza kwa Machali kuhama chama, ambapo awali alikuwa CHADEMA, kisha akahamia NCCR mageuzi na mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu alijiunga na ACT Wazalendo ambako amedumu kwa takriban mwaka mmoja, na sasa amejiunga CCM

No comments:
Post a Comment