CCM ina miaka 39 tangu izaliwe na imekuwa madarakani wakati wote huo, lakini mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe anaona chama hicho kinasumbuliwa na matatizo manne ambayo kama mwenyekiti wake, John Magufuli atayaondoa, kitakuwa imara zaidi.
Unafiki na majungu, udhibiti wa rasilimali za chama, mfumo mbovu wa kupata viongozi na kutokuwapo na mfumo wa kulinda haki za wanachama ni mambo ambayo Bashe anaona yanaisumbua CCM na yatamsumbua mwenyekiti huyo mpya ambaye amejipambanua kama mtu anayetaka “kuinyoosha nchi”.
Bashe, ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka jana baada ya jaribio lake la kwanza mwaka 2010 kukumbana na kikwazo cha urais ndani ya CCM, alisema hayo Ijumaa katika mahojiano maalumu .
“Akifanikiwa kutekeleza haya, atakuwa amefanya kitu bora zaidi,” alisema Bashe ambaye alimsifu Magufuli kuwa ni kiongozi jasiri anayethubutu kufanya mambo ambayo watu hawatarajii.
No comments:
Post a Comment