HABARI, BIASHARA, MUSIC, SIASA, MICHEZO,

Monday, 14 November 2016

KIONGOZI WA M23 ATOROKA KAMBINI


KIONGOZI wa zamani wa kundi kubwa la waasi wa M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Sultani Makenga ametoroka kambini Uganda.
Kutokana na tukio hilo, DRC imeimarisha doria za kijeshi katika eneo tete la mashariki mwa nchi.
Imeripotiwa kuwa milio ya risasi ilisikika nje ya mji muhimu wa mpaka wa nchi hizo mbili
Gavana wa Mkoa wa Kivu Kaskazini, Julien Paluku amesema maafisa wa Uganda hawafahamu aliko kiongozi huyo.
Akizungumza na Shirika la Habari la Reuters, Paluku alisema wamewasiliana na idara ya Ujasusi ya Uganda ambako wamethibitisha tangu Ijumaa mwanajeshi huyo wa zamani mwenye chao cha ukanali hajulikani aliko na huenda ametoroka.
Afisa mmoja wa M23 kutoka tawi la kisiasa la kundi hilo amekataa kusema chochote kuhusiana na suala hilo na badala yake amesema suala hilo waulizwe maafisa wa Uganda.

Mapigano ya risasi yalitokea katika mji wa mpakani wa Bunagana, ambao uliwahi kuwa ngome ya M23 usiku wa Ijumaa hadi Jumamosi asubuhi.

No comments:

Post a Comment