Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata
Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa mrithi wake kuongoza
serikali ya mpito.
Kujiuzulu kwa bwana Ponyo ni sehemu ya
makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita kati ya serikali ya Rais
Joseph Kabila na baadhi ya vyama va upinzani ya kuhairisha uchaguzi wa
urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.
Wapiga kura nchini DRC
walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati
wa kumalizika kwa mhula wake wa mwisho.
Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu na bwana Ponyo.
No comments:
Post a Comment