Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Augustine L. Ollomi kupitia kipindi cha Adhuhuri Lounge cha Azam TV amesema, kifo cha mchezaji wa U-20 wa Mbao FC kilitokana na moyo kusimama ghafla (Sadden Cardiac Arrest).
“Tumepokea taarifa kutoka kwa askari wetu ambao walikuwa wanaangalia usalama pale uwanjani ambapo kulikuwa na mechi kati ya Mbao FC kutoka Mwanza na timu nyingine ya Mwadui FC.”
“Kuna mchezaji alianguka wakati wanagombea mpira na mchezaji mwenzie kwahiyo akawa amepata mshtuko, alikimbizwa hadi hospitali ya Rufaa ya mkoa muda kama wa saa 12:08 lakini baada ya uchunguzi ikagundulika kwamba ameshafariki dunia.”
“Tulifungua jalada la uchunguzi, bahati nzuri madaktari walitufanyia huduma ya haraka, kwa muonekano huyu Bw. Ismail Mrisho Khalfan ambaye ndio alikuwa ameanguka pale uwanjani kwa nje hakuonekana kuwa na jeraha kwa hiyo madaktari wakatueleza lazima afanyiwe uchunguzi wa kina.”
“Matokeo yake ni kwamba, daktari alituthibitishia kwamba, kifo kilitokana na moyo kusimama ghafla (Sadden Cardiac Arrest).”
No comments:
Post a Comment