Baada ya jana kijana Ismail Mrisho kufariki dunia uwanjani wakati akiitumikia klabu yake ya Mbao FC U20 dhidi ya Mwadui FC, taarifa kutoka mjini Bukoba zinasema kijana huyo atazikwa leo jioni nyumbani kwao jijini Mwanza.
Mwili wa marehemu tayari umeshasafirishwa kwenda jijini Mwanza ambako ndipo nyumbani kwao maremu. Msiba utakua eneo la Dampo karibu na chuo cha Mount Meru huku mazishi yakitarajiwa kufanyika leo majira ya saa 10 jioni.
Mechi zote za kituo cha Bukoba ambazo zilikuwa zinatarajiwa kuchezwa leo zimeahirishwa kupisha msiba huo.
No comments:
Post a Comment