Manchester United ililazimishwa suluhu na Liverpool kwenye uwanja wa Anfield.
Mchezo huo unadaiwa haukuwa wa kuvutia kama ilivyokuwa kwa mechi za Liverpool v Manchester United miaka michache iliyopita.
Timu zote zilipambana kusaka ushindi lakini inaonesha chini ya JJose Mourinho mipango ya kikosi chake ilikuwa ni kuzuia kufungwa goli kuliko kushambulia na kuhakikisha ushindi unapatikana.
Kukiwa na nafasi chache za kufunga kutoka kila upande mashabiki hawakupata burudani waliyoitarajia kutoka kwa timu zao.
Matarajio ya wengi hayakutimia kutoka katika mchezo huo huku wengine wakichukizwa na viwango vya mchezaji mmoja-mmoja
Mchezaji ambaye ametupiwa lawama na mashabiki wengi ni kiungo wa Manchester United Paul Pogba.
Mfaransa huyo ambaye ada yake ya usajili ilikuwa ni £89 milioni wakati wa majira ya usajili uliopita wa majira ya joto bado hakuonesha thamani yake uwanjani ukilinganisha na kitita kilicholipwa kumnunua.
Bado hajaweza kucheza kwa mwendelezo wa kiwango cha juu huku akiwa amefunga goli moja tangu aliporejea Old Trafford.
Kiwango chake katika mchezo dhidi ya Liverpool hakikuwa cha kuridhisha na mashabiki wengi walishindwa kujizuia na kuamua ku-post mitazamo yao kwenye mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment